Tuesday, January 19, 2016

MWANA FA AJA NA REMIX YA ASANTENI KWA KUJA

Mwana FA amesema mapokezi makubwa ya wimbo wake mpya ‘Asanteni Kwa Kuja’, imemfanya aandae remix ya wimbo huo.


FA amesema kama angepata nafasi ya kumuongeza Professor Jay kwenye remix hiyo angetisha zaidi.
“Ukiona wasanii wameikubali na kila mmoja anajaribu kuweka namna yeye angeifanya Asanteni kwa kuja ni kitu kizuri sana,”FA aliiambia 255 katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumanne hii. “So kweli nafikiria kufanya remix, ikiwezekana nifanye hata mbili tatu kama mtoni vile watu wanavyofanya.”
“Nafikiri Fid Q alidondokea vizuri kwenye hii beat, Jay MoE aliiua sana na Solo. Lakini ningekuwa na uwezo wa kumpata mheshimiwa mbunge Professor ingekuwa vizuri sana lakini hao watatu ndio ninao mpaka sasa.”
FA amesema angependa pia kumtupia muimbaji wa kike.
“Mtu kama Maua Sama au Vanessa Mdee ingekuwa shoka zaidi.”

No comments:

Post a Comment