Picha 5 za bibi wa miaka 54 aliyeingia kwenye headlines za kuusaka umiss Uingereza
on
January 17, 2016
Uingereza kuna mashindano ya urembo yamepewa jina la Miss Galaxy, unaambiwa bibi mmoja Amanda Booth kaona hata asipitwe na hii, na yeye kaingia kama mmoja wa wanaosaka Taji hilo japo umri wake ni miaka 54 na ameingia kugombea Taji hilo na warembo wengine ambao umri wao ni miaka 20 !!
Waandaaji wa shindano hilo wamesema bibi huyo amevunja rekodi kwa kama miaka 20 hivi iliyopita hakuwahi kutokea mrembo anayeshiriki mashindano hayo mwenye umri mkubwa kama wake… ilikuwa ndoto yake kufanya masuala ya urembo, lakini ndoto hiyo kaitimiza sasa kushiriki shindano hilo.
Hii ni picha ya bibi huyo alipokuwa na umri wa miaka 25
No comments:
Post a Comment